ZRB YATEKELEZA AZIMIO LA KUIMARISHA USTAWI WA MTOTO

Katika kutimiza maazimio ya mkataba wa umoja wa mataifa kuhusu kuimarisha ustawi wa mtoto bodi ya mapato Zanzibar ZRB imetekeleza azimio hilo kwa kutoa msaada wa magodoro na vitabu katika kituo cha kulelea watoto yatima mazizini ikiwa ni kutimiza ahadi waliyoitoa kwa kituo hicho.

Akikabidhi msaada huo mwenyekiti wa bodi ya ZRB Nd. Saleh Osman Sadiq amesema ZRB kutokana na uundwaji wake inasaidia changamoto nyingi zinazowakabili wananchi hivyo imetoa msaada huo ili kuona watoto hao wanalelewa katika mazingira ya kuridhisha.

Naibu katibu Mkuu wizara ya kazi, uwezeshaji, wazee, wanawake na watoto Nd. Mwanajuma Majid amesisitiza bodi hiyo na taasisi nyengine kwa pamoja kuzidisha juhudi za kustawisha maisha ya watoto katika jamii ili kujenga taifa imara litakalokuwa na vijana wenye imani thabiti ya kuipenda nchi na raia wake.

 

Comments are closed.

error: Content is protected !!