ZFF YAITAKA TFF KUWAPA RUZUKU ZAO KUTOKA FIFA

Shirikisho la  soka Zanzibar ZFF  limelitaka shirikisho  la soka Tanzania TFF  kuhakikisha  wanawapa ruzuku  zao zinazotoka  katika shirikisho la soka la dunia FIFA  kama inavotakiwa .

Akizungumza na waandishi wa habari  katika ukumbi  wa shirikisho hilo  Amani mjini Zanzibar  msemaji mkuu wa shirikisho la soka Zanzibar Adam Natepe  amesema  ZFF haina matatizo yoyote  wala mgororo na TFF kinachotakiwa  ni ZFF kupewa haki yao.

Aidha  afisa huyo wa habari amesema  mbali na suala hilo pia  wanazidai klabu  za tanzania bara milioni 19 ambazo pesa hizo zinatokana na uhamisho  wa wachezaji 19  waliohama kutoka timu mbalimbali hapa visiwani na kujiunga na klabu za Tanzania bara ambapo kila mchezaji mmoja katika uhamisho wake inatakiwa itoke shilingi milioni moja.

Shirikisho la soka Zanzibar linaidai TFF dola laki nne.

Comments are closed.

error: Content is protected !!