ZECO YAKABIDHI SHILINGI MILIONI MOJA KWA TIMU YA TAIFA YA ZANZIBAR.

Shirika la Umeme Zanzibar ZECO limekabidhi shilingi milioni moja kwa timu ya Taifa ya Zanzibar [Zanzibar Heroes] ikiwa nimchango wa shirika hilo kwa ajili ya maandalizi

Akizungumza na waandishi wa habari za michezo mara baada ya kukabidhi fedha meneja wa uhusiano na huduma kwa wateja Zanzibar Salum Abdallah Hasani amesema ni jukumu la kila moja kuona ipo haja ya kuweza kuichangia timu hiyo ili kuweza kufanikisha malengo waliyo jiwekea.

Akipokea pesa hizo mwenyekiti wa kamati ya hamasa Ayoub Moh’d Mahamoud ameshukuru kwa Shirikia hilo kujali uzalendo wa taifa kwa kuweza kuwa sehemu ya kufanikisha malengo yaliyo kusudiwa.

Comments are closed.

error: Content is protected !!