ZAIDI YA ASILIMIA 50 YA WANAWAKE TANZANIA WANAUGUA SARATANI YA KIZAZI

Zaidi ya asilimia 50 ya wanawake tanzania wanaugua saratani ya kizazi na kati yao asilimia 34.4 hufariki dunia kila mwaka kutokana na ugonjwa huo.

Hayo yameelezwa na dk issa omar khamis ambae ni daktari mkuu katika hospitali ya maida charitable health foundation iliyoko fuoni ijtimai katika kikao cha tathmini cha mwisho wa mwaka kilichoenda sambamba na utoaji wa elimu ya lishe na afya ya uzazi kwa kinamama pamoja na elimu ya saratani ya kizazi.

Amesema kinamama wanahitaji kufanya uchunguzi wa saratani ya kizazi kila baada ya miaka mitatu kwa waliokuwa hawajaathirika na vvu na walioathirika na vvu kila baada ya mwaka mmoja chini ya usimamizi wa kina baba kwani katika sababu zinazopelekea ugonjwa ni kuzaa watoto wengi.

Mwenyekiti wa jumuiya maida charitable health foundation kassim issa kirobo amesema lengo la kuanzishwa kwa jumuiya hiyo ni kuisaidia jamii hasa wanawake na watoto kwa kutoa huduma bure za mama mjamzito na mtoto alie chini ya umri wa miaka mitano ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali ya mapinduzi ya zanzibar chini ya uongozi wa rais dk ali mohammed shein.

Mratibu wa mama na watoto kutoka jumuiya  hiyo amesema pamoja na kutoa huduma hizo pia taasisi hiyo inatoa elimu ya uzazi, lishe pamoja na saratani ya kizazi na pia ina mpango wa kutanua huduma hizo ili kuhakikisha kina mama wanahudhuria cliniki kwa wakati kwa ajili ya kujua afya zao.

No Comments Yet.

Leave a comment