WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO KUTOA HUDUMA BORA NA ENDELEVU KWA MASLAHI YA NCHI NA WANANCHI.

Wizara ya fedha na mipango imesema itaendelea watendaji wa Wizara hiyo katika utendaji wao wa kazi kulingana na mkataba ya huduma kwa wateja ili kutoa huduma bora na endelevu kwa maslahi ya nchi na wananchi wake.

Mkurugenzi uendeshaji na utumiashi wa wizara hiyo Ali Bakar Is-haka akifungua mkutano wa mapitio ya mkataba wa utoaji huduma kwa umma amesema mkataba huo umeweka wazi majukumu wajibu na haki katika kuwahudumia wananchi hivyo utekelezaji wa majukumu kupitia mkataba huo kutasaidia kuondoa malalamiko kwa wananchi.

Akiwasisha mada juu ya umuhimu wa mkataba wa huduma kwa wateja afisa uchambuzi kazi mwandamizi kutoka ofisi ya Rais utumishi wa umma na utawala bora Othman Simba Makame amezishauri taasisi za Serikali kufanya mapitio ya mikataba yao kila mwaka ili kuboresha mapungufu yanayojitokeza katika utoaji wa huduma.

Washiriki wa mkutano huo wamesema licha ya elimu waliyoipata bado kuna umuhimu mkubwa wa kuufikisha mkataba huo kwa wananchi ili ili kuwajengea uwezo wa kujenga hoja katika katika kutetea haki zao pale wanaponyimwa huduma wanazostahiki.

 

Comments are closed.

error: Content is protected !!