WIZARA YA AFYA IMEWATOA HOFU WANANCHI KUWA HAKUNA KESI YA UGONJWA WA EBOLA ILIYORIPOTIWA ZANZIBAR.

 

Wizara ya Afya imewatoa hofu Wananchi kuwa hakuna kesi ya ugonjwa wa Ebola iliyoripotiwa Zanzibar.

Mkurugenzi wa idara ya kinga na elimu ya Afya Nd; Juma Salum Mbwana ameeleza hayo katika mafunzo ya Ebola kwa Waandishi wa Habari Zanzibar.

Nd; Juma amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwaelimisha Wanahabari juu ya kutoa taarifa kwa Wananchi juu ya kujikinga na ugonjwa huo na kwamba hadi sasa ugonjwa huo haujaripotiwa Zanzibar.

Mkuu wa kitengo cha Elimu ya  Afya  Zanzibar Nd; Halima Ali Khamisi amesema elimu hiyo ya kinga ya Ebola inapaswa iwafikie wananchi wote hivyo Waandishi wa Habari wana jukumu kubwa la kuifikisha Elimu hiyo kwa wananchi ili wachukue tahadhari.

Katika mafunzo hayo pia yameshirikisha igizo la kujikinga na maambukizo ugonjwa huo wa Ebola.

 

Comments are closed.

error: Content is protected !!