WIZARA YA AFYA IMETILIANA SAINI YA MAKUBALIANO KATI YA MADAKTARI WA KICHINA WALIOPO ZANZIBAR

Wizara ya Afya imetiliana saini makubaliano maalum na Jamhuri ya Watu wa China juu ya utaratibu wa Madaktari wa Kichina wanaofanya kazi katika Hospitali za Mnazi Mmoja na Abdalla Mzee.

Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Asha Ali Abdalla Amesema makubaliano hayo yametokana na mabadiliko madogo yaliyofanyika katika utaratibu wa kufanya kazi Zanzibar Madaktari hao katika gharama za Usafiri.

Amesema ushirikiano mzuri wa China na Zanzibar katika sekta ya Afya ikiwemo kuwajengea uwezo Madaktari na watendaji wa Wizara hiyo umesaidia Hospitali za Zanzibar kutoa Huduma bora kwa Wananchi

Balozi Mdogo wa China aliyepo Zanzibar Xie Xiaowu amesifu Zanzibar kwa mafanikio makubwa iliyoyapata katika miaka 56 hasa katika sekta ya Afya ambayo yametokana na ushirikiano mzuri na juhudi za Rais wa China Xi Jinping ya kusaidia maendeleo ya Bara la Afrika ikiwemo  Zanzibar.

Comments are closed.

error: Content is protected !!