WAZIRI MKUU AMEWATAKA WANANCHI KUWAPIGIA KURA WAGOMBEA WA NGAZI ZOTE WA CCM IFIKAPO OCTOBER 28

Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim  Majaliwa Amesema katika kipindi hichi cha  Kampeni  za kuelekea Uchaguzi Mkuu Wananchi wanatakiwa  kufanya  tathmini  ya  hali  ilivyokuwa awali na ilivyo sasa ili waweze kufanya Maamuzi sahihi.

Amesema endapo watafanya tathmini vizuri anaimani kuwa watajitokeza kwa wingi Siku ya Tarehe 28 Oktoba Kuwapigia Kura Wagombea wa Ngazi zote wa Chama cha Mapinduzi  kwani  ndio Wagombea pekee wenye Uwezo wa kuwatumikia vizuri.

Akifungua Bima ya Mbio za Masafa Marefu ya Benki Nmb “Nmb Bima Marathon kwa Mwaka 2020, Mhe.Majaliwa Amesema katika kuhakikisha  maendeleo  makubwa zaidi yanafikiwa ni  muhimu kuendelea kudumisha upendo, Amani na Mshikamano katika Kipindi hichi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu na hata baada ya Uchaguzi.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amesema Serikali imewekeza Shilingi Milioni 75 kwa Ajili ya kuongeza Vitanda kwa huduma ya Matibabu ya Tiba Kemia kutoka Vitanda 40 hadi Vitanda 100 kwa sasa.

Pia Mhe.Majaliwa ametumia fursa hiyo kuipongeza Benki ya Nmb kwa kwenda sambamba na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano, inayoongozwa na Rais Dkt. Magufuli hasa  kwenye kupitisha huduma za Kifedha jumuishi kwa Jamii, ikiwemo kurahisisha upatikanaji wa Bima kupitia Mtandao wao mpana wa Matawi 226 Nchini.

 

 

 

Comments are closed.

error: Content is protected !!