WAWEKEZAJI WA HOTELI ZA KITALII WAMESISITIZWA KUFUATA NA KUTII SHERIA ZA NCHI

Wawekezaji wa Hoteli za Kitalii wamesisitizwa kufuata na kutii sheria za za Nchi ili kuepusha usumbufu unaoweza kujitokeza kutokana na ukiukwaji wa  sheria  unaofanywa na  baadhi  yao katika kuendesha shughuli  za  Utalii.

Akizungumza wakati akikabidhi tamko la serikali kwa wawekezaji wa Hoteli hizo lenye lengo la kuwakumbusha juu ya utii wa sheria za Nchi Mkurugenzi wa uwekezaji wa ZIPA  Sharif Ali Sharif amesema Serikali imechukuwa hatua  hiyo jiti baada ya kuona changamoto za ukiukwaji wa sheria kwa baadhi ya wawekezaji zinazo sababisha usumbufu kwa  Wananchi  na  upotevu wa  mapato  ya  Serikali.

Wakati huo huo Nd. Sharif amekemea vikali na kuahidi  kuwachukulia hatua wawekezaji waliodharau  ujumbe  huo wa Serikali  na  kuamua kuondoka katika maeneo  yao  ya  kazi.

Akitoa maelezo juu ya tamko hilo la Serikali kwa wawekezaji  Mwanasheria wa Serikali  kutoka ZIPA     Nd. Shida Makame amesema miongoni mwa sheria zinazotakiwa kuwekewa mkazo ni pamoja na kutokuweka vikwazo katika matumizi  ya Ufukwe kwa Wananchi na Watumishi wa Serikali, ulipaji kodi na  utunzaji wa Mazingira, sheria za kazi na nyengine wanazo  husika  nazo.

Baadhi  ya  wawekezaji hao wameiomba Serikali kuchukuwa hatua zinazostahiki pindi wanapowasilisha kero  ambazo huathiri Biashara ya Utalii pamoja na kusababisha kutokuelwana  na  jamii.

 

Comments are closed.

error: Content is protected !!