WATUMISHI WA UMMA KUFANYAKAZI KWA KUFUATA SHERIA NA KUACHA KUFANYA KAZI KWA MAZOEA

Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Mh. Othman Masoud Othman amewataka Watumishi wa Idara zilizomo kwenye Afisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais kufanya kazi kwa kufuata  misingi ya sheria na kanuni za Utumishi ili kutoa huduma kwa jamii ipasavyo.

Mh. Othman ameyasema hayo katika kikao na Wafanyakazi wa idara zilizo chini ya Ofisi yake Kisiwani Pemba mara baada ya kuzitembelea idara hizo Gombani Chakechake .

Amesema ni wajibu wa kila Mtumishi wa Umma kufanyakazi kwa kufuata Sheria na kuacha kufanya kazi kwa mazoea kwani serikali za awamu ya nane imekusudia kutoa huduma kwa jamii bila kuwepo kwa urasimu .

Aidha mh. Othman amesema katika kuyafikia malengo hayo ni lazima Wafanyakazi kuongeza ubunifu kupia taaluma zao kwa kuyatangaza mambo yanayotekeleza  kwa kuandaa vindi katika vyombo vya habari zikiwemo mitandao ya kijanmii .

Amesema kwamba zimo Taasisi ikiwemo ya mazingira ambazo zinaweza kuielimisha Jamii kupia vyombo hivyo namna ya kuhifadhi mazingira pamoja kitengo cha madawa ya kulevya kutoa elimu ya kupambana na janga hilo kwa vijana ambao ndio nguvu kazi ya Taifa.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamo wa kwanza wa Rais  Khadija Khamis Rajab amesema  Ofisi  inaendelea kuzipatia ufumbuzi wa haraka  changamoto  zinazowakabili  ili malengo waliojipangia  yaweze kufikiwa wakati .

Comments are closed.