WATENDAJI WAPYA WA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR WASISITIZWA KUACHA DHARAU WANAPO HUDUMIA JAMII

Watendaji wapya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wamesisitizwa kuacha kudharua makundi mengine ya kijamii wanapotoa huduma katika taasisi zao.

Amesema makundi hasa ya watu wenye walemavu wamekuwa wakipata tabu wanapohitaji huduma muhimu na kufikiriwa kuwa si miongoni wa sehemu ya jamii.

Mkuu wa idara ya mafunzo mafupi Mw.Abdallah Juma akifunga mafunzo elekezi kwa watumishi hao wapya amesisitiza uzalendo na uwajibikaji ili kuleta ufanisi kwa taasisi na idara za serikali.

Nao watumishi wapya waliopatiwa mafunzo hayo yaliyoandaliwa na chuo cha utawala wa umma wameahidi kuleta mabadiliko ya kiutendaji kwa kuongeza ari ya kazi.

Comments are closed.

error: Content is protected !!