WATAKAOTUHUMIWA KUHUSIKA NA VITENDO VYA RUSHWA WATASIMAMISHA KAZI ILI KUPISHA UCHUNGUZI

Rais wa Z anzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema Viongozi wote wa Utumishi wa Umma watakaotuhumiwa kuhusika na vitendo vya Rushwa pamoja na ukiukwaji wa Maadili, watasimamisha kazi ili kupisha Uchunguzi.

Dk. Mwinyi amesema hayo leo katika ukumbi wa Sheikh Idrisa abdul-Wakili Kikwajuni Jijini hapa, wakati alipozungumza na Viongozi, watendaji na wafanyakazi wa Utumishi wa Umma katika kilele cha maadhimisho ya siku ya maadili na haki za binadamu.

Amesema mara tu baada ya kuingia Madarakani, Serikali imeanza kuwachukulia hatua za kisheria Viongozi wasiowajibika na wasioshikamana na maadili ya kazi zao, kufuatia ziara zilizofanyika katika Taasisi mbali mbali, ikiwemo bandari, Hospitali ya Mnazi Mmoja na maeneo mengine yaliomo katika mpango wa utekelezaji wa mradi wa kuendeleza huduma mjini (ZUSP).

Alisisitiza na kurejea maelezo aliyoyatoa kwa nyakati tofauti dhidi ya watendaji waliohusika au kutiliwa shaka ya kuhusika na vitendo vya Rushwa na ukiukwaji wa maadili; kuwa Serikali nayoiongoza itakabiliana ipasavyo na vitendo vyote vinavyoathiri utekelezaji wa misingi ya Utawala bora.

Alisema anafurahishwa na hatua ya Wananchi ya kuiunga mkono Serikali na kubainisha kuwa yeyote yule atakeatuhumiwa na hatimae kubainika hana kosa, atarejeshwa kazini na kupata haki zake kama sheria zinavyoelekeza.

“kiongozi wa umma lazima afanye kila linalowezekana kuwa mfano na kigezo cha tabia njema na ajiepushe hata na vitendo vinavyoweza kumfanya atiliwe shaka”, alisema.

Dk. Mwinyi alisema ni jambo la kusikitisha kuona taarifa iliyowasilishwa kwake kutoka zaeca , kuonyesha kuwepo tatizo kubwa la ubadhirifu wa mali za serikali na wizi katika utekelezaji wa miradi mikubwa.

Hata hivyo alisema amefurahishwa na kazi inayoendelea ya ufuatiliaji, hivyo akawataka viongozi wote watakaotuhumiwa kuhusika na ubadhirifu huo kutoa ushirikiano wa kisheria kwa chombo hicho.

“nimevutiwa sana na ari na utayari wa watendaji wa zaeca katika kufanikisha vita dhidi ya rushwa na ubadhirifu wa mali ya umma, tutayazingatia maombi yao waliyotueleza” , alisema.

Aidha, alisema anatambua hatua zinazoendelea kuchukuliwa na serikali kuwa hazitowafurahisha watu wote, hivyo akawataka wananchi kuikubali hali hiyo kwa msingi kuwa wengi wataguswa, akibainisha nchi kugubikwa na muhali.

Alisema kuna miradi kadhaa mikubwa inayoonyesha kuwepo matumizi makubwa ya fedha, ambazo hazikutumika vyema (kwa mujibu wa taratibu).

Alisema wale wote watakaobainika kuhusika na uzembe, wizi au ubadhirifu wa mali ya umma, mahala popote walipo; watachukuliwa hatua  na  kusitiza azma ya seriklai katika kuzingatia haki na kuepuka maonevu.

Alipongeza kazi kubwa iliofanywa na awamu zote za serikali zilizotangulia ya kuunda taasisi na kutunga sheria zilizo bora katika kufanikisha dhana  ya uimarishaji  utawala bora, akinasibisha hatua hiyo kuwa ni ujenzi wa miundombinu iliyo bora.

Alieleza kuwa serikali imefanikiwa kuanzisha ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka, idara ya utawala bora, mamlaka ya kuzuia rushwa na uhujumu uchumi, tume ya maadili ya viongozi wa umma pamoja na kuimarisha ofisi ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ili kutekeleza majukum yake kwa ufanisi.

Aliwataka washiriki wa mkutano huo kuyatumia maadhimisho hayo kutafakari umuhimu wa kuendeleza maadili mema ndani ya jamii, sambamba na kupiga vita vitendo vya udhalilishaji wa watoto na unyanyasaji wa kijinsia.

Aidha, aliwataka kushirikiana na jamii katika kuyakomesha vitendo hivyo pamoja na kuendeleza matumzii mazuri ya mitandao, sambamba na kupiga vita utumiaji wa dawa za kulevya.

Mapema, waziri wa nchi (or) katiba,sheria,utumishi wa umma na utawala bora haroun ali suleiman, alitowa wito kwa wananchi  kuunga mkono juhudi za rais wa zanzibar katika kuimarisha utawala bora pamoja na kulaani kwa nguvu zote vitendo vya rushwa.

Aidha, aliwataka watumishi wote wa serikali kudhibiti siri za serikali na kubainisha hatua zitachukuliwa dhidi ya watumishi wasio waaminifu watakaovujisha siri hizo.

 

Viongozi mbali mbali wa kitaifa na kijamii walihudhuria mkutano huo, akiwemo makamo wa kwanza wa rais maalim seif sharif hamad, makamo wa pili wa rais hemed suleiman abdalla, katibu wa baraza la mapinduzi na katibu mkuu kiongozi dk. Abdulhamid yahya mzee, jaji mkuu wa zanzibar omar othman makungu, mwanasheria mkuu wa zanzibar dk. Mwinyi talib haji, mawaziri, wakuu wa vikosi vya smz, viongozi wa vyama vya siasa, viongozi wa dini pamoja na wafanyakazi wa utumishi wa umma.

 

 

 

 

 

 

Comments are closed.