WASANII WA TASNIA YA FILAMU ZANZIBAR WAMEHIMIZWA KUWA NA TAALUMA YA UPIGAJI PICHA KATIKA FILAMU ZAO

Wasanii wa Tasnia ya Filamu Zanzibar, Wamehimizwa kuwa na Taaluma ya Upigaji Picha kwenye Filamu zao kwa madhumuni ya kuzalisha Filamu zenye ubora.

Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Zanzibar ambae pia ni Mkufunzi  wa Mafunzo yanayondelea hapa ZBC, amewambia Wasanii kwamba katika kuzalisha Filamu zenye kiwango ni vyema kwa msimamizi Mkuu wa Filamu akaandaa mwenendo mzima wa kazi kimaandishi, huku wakizingatia suala la mashirikiano kwa wenye mamlaka katika maeneo wanayokwenda kurekodi Filamu zao.

Katika maoni yao Wasanii hao wamesema hali ngumu ya fedha inachangia kwa kiasi kikubwa kuzalisha Filamu zisizo fikia viwango vya Kimataifa.

Mafunzo hayo ya siku 10 yameandaliwa na Ofisi ya haki Miliki Zanzibar kwa malengo ya kuwaongezea uwezo waandaaji wa Filamu Zanzibar.

 

 

Comments are closed.

error: Content is protected !!