WASANII WA TASNIA YA FILAMU NCHINI WAMETAKIWA KUJIONGEZA KITAALUMA

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo   Nd.Amour Hamil Bakar Amewasisitiza Wasanii wa Tasnia ya Filamu Zanzibar kujiongeza Kitaaluma ili wapate fursa za kujifunza zaidi nafasi inapotokezea.

Akifunga Mafunzo ya Siku Kumi ya kuwajengea uwezo Wasanii Waandaaji wa Filamu pamoja na Waandishi wa Filamu Zanzibar Naibu Katibu Mkuu huyo Amesema Zanzibar ina Fursa ya kuwa na Wasanii wenye Uwezo wa kuzalisha Filamu zenye Viwango, ila kinacho wakwamisha ni uhaba wa Taaluma ya Tasnia hiyo.

Msimamizi na Mtendaji Mkuu wa Ofisi ya Cosoza Zanzibar Ndugu Mtumwa Khatib Ameir, Amesema endapo Wasanii hao  wataitumia Taaluma walioipata katika Mafunzo hayo ya Siku 10 itawasaidia kukuza kipato cha Wasanii hao.

Wakufunzi wa Mafunzo hayo wamesema kazi za Wasanii hao zinaweza kuwa za Kimataifa iwapo Watapata Mafunzo ya ziada katika masuala ya Taa, Uungaji Picha na Sauti.

Washiriki wa Mafunzo hayo wameipongeza Taasisi ya Cosoza pamoja Wakufunzi wa Mafunzo hayo na kusema kuwa ni imani yao kuwa Mafunzo waliopatiwa, yamewaongezea Ujuzi zaidi na ni Matumaini yao kuwa Watafanya kazi zenye Ubora wa hali ya juu.

 

 

Comments are closed.