WASANII NCHINI WAMETAKIWA KUSAJILI VIKUNDI VYAO ILI KUFAIDIKA NA FURSA ZITAKOZOJITOKEZA

Baraza la Sanaa,Sensa ya Filamu na Utamduni Zanzibar limewataka Wasanii mbalimbali Nchini kusajili vikundi vyao ili kufaidika na fursa zitakazojitokeza ndani na nje ya nchi katika kukuza kazi zao.

Akizungumza na wasanii wa Wilaya ya Kati katika mafunzo kwa wasanii hao katibu mtendaji wa Baraza la Sanaa, Sensa ya Filamu  na Utamaduni Zanzibar Dk Omar Abdallah Adam amesema ili msanii au kikundi cha wasanii kufikia mafanikio anawajibu wa kujisajili katika taasisi husika kwa ajili ya kunufaika na fursa zinazojitokeza kwa wasanii hao.

Amesema miongoni mwa fursa ambazo msanii anaweza kuzipata baada ya kujisajili  ni kushiriki katika matamasha mbali mbali ya ndani na nje, kukuza kipato cha wasanii na kuweza kupatiwa elimu kwa mujibu wa mabadiliko yaTekenolojia Duniani.

Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo wameelezea kufurahishwa na mafunzo waliopatiwa kwani yatawajengea uwezo wa kujiamini wakati wa uwasilishaji wa kazi zao  kwa jamii

Comments are closed.