WAPANGAJI WA NYUMBA ZA MICHENZANI WAMELISHAURI SHIRIKA LA NYUMBA KUIMARISHA MAZINGIRA YA NYUMBA HIZO

Wapangaji wa nyumba za maendeleo michenzani wamelishauri shirika la nyumba kuimarisha mazingira ya nyumba hizo kutokana na kasi ya mabadiliko ya miji.

Wakizungumza katika mkutano wa kujadili rasimu ya mkataba wa huduma za umma uliofanyika rahaleo wameeleza kuwa kufanyahifo kutasaidia kuimarisha majumba hayo mamoja na kuleta haiba katika mazingira ya mjini.

Mkurugenzi mkuu  wa shirika la nyumba Zanzibar Bi Riziki Jecha Salim amewataka wananchi wanoishi katika nyumba za maendeleo kuzitunza nyumba hizo pamoja na kufuata sheria za shirika la nyumba.

Akiwasilisha mada juu ya mkataba wa huduma kwa umma na mambo mengine yanayohusiana na hayo kaimu mkurugenzi utawala na rasilimali watu kutoka shirika la nyumba Zanzibar Bi Mwantum Ramadhan Mussa amesema wajibu wa mkataba  ni pamoja na kutoa taarifa sahihi na kwa wakati na kutoa huduma bora kwa walengwa.

Washiriki wa mkutano akiwemo sheha wa shehia ya Rahaleo Bi Mwanakheir Sultan na bwana Mohamed Mugheir wameomba watendaji wa shirika hilo kutoa taarifa kwa masheha pindi wanapotoa mikataba kwa wapangaji ili kuepusha usumbufu.

 

Comments are closed.

error: Content is protected !!