WANDISHI WA HABARI KUACHA USHABIKI WA VYAMA VYA SIASA KATIKA KIPINDI UCHAGUZI MKUU

Baraza la Habari  Tanzania MCT limewakumbusha  Wandishi wa Habari  kuacha ushabiki wa  vyama vya siasa katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu unaorajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi ujao.

Limesema watendaji hao wanapaswa kufanyakazi kwa mujibu wa maadili ya fani zao ili kuwafanya waaminiwe na wanaowaandikia habari zao pa,moja na Jamii kwa jumla.

Akizungumza katika mkutano  na watendaji hao

Mjumbe wa Bodi ya Baraza hilo ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya MCT Bwana Juxon Isaak akizungumza na Watendaji wa Shirika la Utangazaji ZBC hapa Karume House  amesema katika kuepuka makosa hayo yasijitokeze amewashauri waandishi wa  kuhakikisha wanafuata  Sheria za Nchi na miongozo yatume za  Uchaguzi.

Mjumbe wa  Kamati ta Maadili ya MCT na Mtangazaji  wa miaka mingi  Bi Edda Sanga  amewataka Wandishi wa Habari na Utangazaji kuipenda kwa dhati kazi hiyo ,kujielimisha zaidi pamoja  kukifanyia utafiti wanachokiandika au kukitangaza.

Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Zanzibar Bi Nasra  Mohd Juma amewataka Wafanyakazi wa ZBC kujenga tabia ya kuipenda kazi yao  hiyo kwa kujituma bila ya kuvunjia moyo  sambamba na kujitafutia  mafunzo madogo  madogo ili kujeiweka katika nafasi nzuri  zaidi.

Ujumbe wa Baraza hilo ulipata nafasi ya kulitembelea  jengo hilo na  kuonyesha  kuridhishwa  na jinsi ya hatua  iliyofikia  baada ya kufanyiwa matengenezo makubwa katika sehemu zake za kurushia matangazo.

 

 

 

 

 

Comments are closed.

error: Content is protected !!