WANANCHI WAMETAKIWA KUTOA MASHIRIKIANO KATIKA KUENDELEZA JUHUDI ZA KULETA MAENDELEO NCHINI

Wananchi wametakiwa kutoa mashirikiano ya kutosha   katika kuendeleza juhudi za kuleta maendeleo nchini. Akizungumza  na ZBC  Waziri wa ardhi nyumba maji na nishati Mh Salama Aboud Twalib wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika ujenzi mpya wa  nyumba ya mfuko wa barabara{ ZURA},kituo cha kupokelea  umeme  mtoni  pamoja na madema ambako kumehifadhiwa vifaa vya kusambazia maji ya ZAWA,amesema kuwa mashirikiano ya wananchi na utendaji mzuri wa  wasimamizi wa sehemu hizo kutasababisha kufikiwa malengo yaliokusudiwa.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa  ZURA  Haji Kali Haji amesema kuwa  ujenzi huo uanotarajiwa kumaliza mwaka huu disemba utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 19.9 za Kitanzania hata hivyo miongoni  mwa faida zilizopatikana kipindi cha ujenzi ni upatikanaji wa  ajira kwa vijana   katika kuendeleza ujenzi huo. Kwaupande wa kituo cha  kupokelea umeme  waziri huyo ametoa wito kwa watendaji  kufanya   kazi kufanya kazi kwa bidii ili kuendelea kutoa huduma nzuri kwa jamii.

 

Comments are closed.

error: Content is protected !!