WANANCHI WA SHEHIA YA MAKANGALE WILAYA YA MICHEWENI WAMESEMA WAKO TAYARI KUPAMBANA NA RUSHWA

wananchi wa shehia ya makangale wilaya ya micheweni wamesema wako tayari kutoa taarifa ya vitendo vya rushwa kwa mamlaka ya rushwa na uhujumu wa uchumi zanzibar (zaeca), lakini malalamiko yao yafanyiwekazi ili wanotuhumiwa watiwe hatiani kisheria.
miongoni mwa wananchi hao ni hassan hamad shaame amekiri kuwepo kwa vitendo hivyo ambayo vinaathiri kiuchumi, kwani yeye binafsi alidaiwa shilingi elfukumi badala ya elfumbili kwa ajili ya cheti cha mtoto wake na huu ni mwaka wa tatu hajakipata.

wananchi wa shehia ya makangale wametowa rai hiyo wakati maafisa za zaeca walipowatembelea katika nyumba zao kwa kuwafanyia mahojiano kupitia dodoso maalumu la kutambua uwelewa wa wananchi juu ya vitendo hivyo na kuwapatia taaluma ya kudhibiti vitendo hivyo.

wamesema sababu za kutokea kwa vitendo vya rushwa ni pamoja na kutaka huduma kwa haraka bila ya kufuata taratibu, hivyo wasimamizi hutumia fursa hiyo kuwadai fedha ya kuwapatia huduma ambayo inatolewa bure.

akielezea lengo la kufanya dodoso hilo mdhamini wa zaeca ofisiya pemba suleiman ame juma amesema ni kutowa taaluma kwa wananchi wa vijijini kuyafahamu majukumu ya zaeca na vipiwataweza kutowa mchango wao katika kukomesha vitendo hivyo

amesema kupitia dodoso hilo wananchi watafahamu aina mbali mbali za vitendo vya rushwa na uhujumu wa uchumi na namna ya kukabiliana navyo bila ya kuwaathiri kiuchumi.

No Comments Yet.

Leave a comment