WANANCHI WA KIJIJI CHA OLE WAMETAKIWA KUSOMA SHERIA ILI KUEPUKA KUCHUKUA HATUA MIKONONI MWAO

Afisa Mdhamini Wizara ya Katiba na Sheria Nd Mattar Zahor amewataka Wananchi wa Ole kujifunza na kusoma Sheria ambapo itawasaidia kuepuka kuchukuwa hatua mikononi mwao pindi inapotokezea migogoro katika jamii.

Nd,Mattar ametowa ushauri huo wakati alipokuwa akizungumza na Wananchi na Wanafunzi   huko katika Skuli ya Msingi Ole  ikiwa ni shamra  shamra za wiki wa msaada wa kisharia na siku ya sheria duniani.

Nae Kamimu Mkurugenzi  kutoka Jumuia ya Wasaidizi wa Sheria Wilaya ya Chake Chake  ,Maalim Mohammed  Hassan  Abdalla  amesema dhamira ya Jumuia  ni kuona   Wananchi  wamekuwa na uwelewa wa kisheria  ili kuona yale makossa ambayo yamo ndani ya Jamii  yanapunguwa  ili kupata Jamii iliyobora.

Pia  Nd,Seif Mohammed Khamis  ambae ni Wakili wa Serikali  wakati akijibu  baadhi ya maswali yaliyoulizwa na Wanachi  amesema tatizo la ucheleweshaji wa utolewaji wa hukumu au kuharibika kwa Kesi za udhalilishaji  inatokana na baadhi ya vitendo hivyo kuchelewa kuripotiwa.

 

Comments are closed.

error: Content is protected !!