WANANCHI WA KIJIJI CHA NUNGWI WAMETAKIWA KUILINDA MIUNDOMBINU WANAYOWEKEWA NA SERIKALI

Wametakiwa kutumia Vyema Miundombinu inayoanzishwa na Serekali au Taasisi Binafsi  kwa lengo la Kujikwamua na Umasikini.

Akikagua maendeleo ya Soko linalojengwa na kufanyiwa Ukarabati kwa baadhi ya Sehemu huko Nungwi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Nd. Omar Ali Amir amewataka Wavuvi kuacha kutumia Vibanda vilivyojengwa kiholela Nje ya Soko hilo ambavyo vinaharibu haiba na Mandhari ya hapo.

Amesema iwapo watalitumia vizuri Soko hilo litaweza kupandisha thamani ya bidhaa zao  na kupata tija  kiuchumi.

Mkurugenzi wa Idara maendeleo ya Uvuvi Nd Mussa Aboud Jumbe amesema Serikali imeamua kuyapatia Ufumbuzi matatizo ya Wavuvi katika Maeneo yao ili kuendesha Harakati zao  na Mazingira bora ya kuuzia Samaki.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uvuvi ya Nungwi kwa Niaba ya Wavuvi Wenzake     Nd.Kibabe Adibu Amesema Soko hilo wameomba kujengewa Uzio  ili liwe katika Mazingira salama.

Soko hilo la Nungwi linafanyiwa Ukarabati na Kujengwa kwa baadhi ya Maeneo chini ya ufadhili wa Mradi wa usimamizi wa Ukanda wa Bahari ya Kusini mwa Bahari ya Hindi na limegharimu zaidi ya Shilingi Milioni 150 kwa  usimamizi wa Serikali Kuu.

 

 

Comments are closed.