WANANCHI KUCHUKUWA TAHADHARI KATIKA KIPINDI HICHI CHA MVUA ZA MASIKA ZILIZOANZA KUJIKINGA NA MARADHI

Mamalaka ya Hali ya Hewa Kanda ya Zanzibar  imewaomba Wananchi kuchukuwa Tahadhari katika kipindi hichi cha Mvua za Masika zilizoanza kujikinga na Maradhi mbali mbali yakiwemo ya  Virusi vya CORONA

Mkuu wa shughuli za Hali ya hewa Zanzibar Nd. Hafidh Juma amesema taarifa za Afya zinaeleza kuwa Virusi vinavyosababisha Maradhi yaCORONA vinasambaa zaidi katika mazingira ya majimaji na baridi ambayo katika msimu huo ndio wakati wake.

Akizungumza na ZBC amesema miongoni mwa tahadhari zinazohitajika kuchukuliwa ni pamoja na kuweka mazingira safi katika makaazi yao hasa kwa kuondosha sehemu zinazotuama maji na kufuatailia taarifa za hali ya hewa mara kwa mara.

Akizungumzia kuhusiana na siku ya Hali ya Hewa Duniani inayoadhimishwa kila ifikapo Marchi 23 amesema Sherehe hizo zimeamuliwa kuahirishwa ili kuungana na agizo la serikali na amewasisitiza wananchi kuchukuwa tahadhari kwani utabiri unaonesha Mvua za Masika zitakuwa kwa kiwango kikubwa.

Amesema Mamlaka hiyo itaendelea kutoa Elimu kwa Jamii juu ya umuhimu wa kulinda Afya zao hasa katika matumizi ya Maji safi inayoendana na kauli mbiu ya mwaka huu ya siku hiyo inayosema Hali ya Hewa na Maji.

Comments are closed.

error: Content is protected !!