WALIMU WAKUU KUSIMAMIA MIPAKA YA SKULI WANAZOZISIMAMIA ILI KUEPUKA UVAMIZI KATIKA MAENEO HAYO

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. Riziki Pembe Juma amewashauri Walimu Wakuu kusimamia mipaka ya Skuli wanazozisimamia ili kuepuka uvamizi katika Maeneo hayo.

Amesema Udhibiti wa Mipaka na kuijengea kuta kutasaidia kulinda maeneo ya Skuli na kuwa katika Mazingira salama.

Akizungumza na Walimu Wakuu Ofsini kwake Mazizini Mhe. Riziki amesema mfano mzuri ulioanza katika Chuo cha Kiislam kwa kujengwa ukuta kutaondosha kero ya uvamizi wa eneo hilo.

Aidha amewataka Walimu kuendelea kushirikiana na Wizara ya Elimu ili kusimamia pamoja na kuweka mikakati bora ya kuondosha vitendo hivyo vya uvamizi Maeneo yao.

Mkuu wa Chuo cha Kiislamu na Wasaidizi wake wamesema mbali ya ukuta huo kulinda mipaka ya Chuo pia unaweka Usalama kwa Wanafunzi hasa wa kike na Mali za Chuo.

 

Comments are closed.

error: Content is protected !!