WALIMU WA MADRASA ZA QUR-AN WAMETAKIWA KUPAMBANA NA MPOROMOKO WA MAADILI

Walimu wa madrasa za Qur-an  kisiwani Pemba wametakiwa kupambana na suala zima la mporomoko wa maadili kwa watoto  ili kuwaepusha na vitendo vya udhalilishaji  kwa ajili ya kuwa na jamii iliyobora.

Ushauri  huo  umetolewa na  Afisa mdhamini wizara ya katiba na Sheria  Nd. Mattar Zahor Massoud wakati akifunguwa mafunzo  kwa walimu wa madrsa  za Qurani  juu ya mbinu bora za kujenga  nidhamu  za wanafunzi ,yaliyoandaliwa na ofisi  ya mufti  huko katika ukumbi  wa ofisi hiyo gombani.

Nae Naibu mufti Zanzibar Shekh Mahmoud Mussa Wadi amewataka walimu  hao katika kutekeleza  majukumu yao kuzingatia  misingi mitatu mikuu ili kuwajenga watoto katika misingi hiyo ikiwemo iimani,kukuza ufahamu  na kuwaelimisha watoto juu  ya makuzi ya mwili kwa mujibu wa umri,elimu na ufahamu wao.

Akitowa  mada  katika mafunzo hayo Shekh Said Khalfan amesema ili malengo ya kuwajenga watoto  katika mwenendo  na tabiia  njema  yaweze kufikiwa  ni lazima pawepo na mashirikiano kati  ya wazazi na walimu.

Katika mafunzo hayo ya siku nne  yaliwashirikisha jumla ya walimu 42 wa madrasa za qurani  kutoka wilaya zote za pemba ikiwa lengo ni kuwawezesha walimu wa mdrasa kufanya shughuli zao kitaalamu

Comments are closed.

error: Content is protected !!