WALIMU KUJIHESHIMU NA KUFUATA MAADILI

Waziri wa nchi afisi ya rais utumishi wa umma na utawala bora mh: haroun ali suleiman amewataka walimu kujiheshimu na kufuata maadili ili lengo la utawala bora liweze kufikiwa.

Akifungua mkutano wa walimu wa somo la uraia mh: haron amesema mwalimu ndio kiyoo katika jamii hivyo si vyema kuwaona wanavunja misingi ya uadilifu katika kazi zao.

Aidha amewataka walimu hao kutumia mbinu ambazo zitawajenga wanafunzi katika misingi ya utawala bora ambayo itasaidia katika kupiga vita kuporomoka kwa maadili.

Akiwasilisha mada ya utawala bora muawasilishaji kutoka idara ya utawala bora nd hassan vui amewataka walimu hao kuwasomesha wanafunzi kwa hisia kwani jitihada zao zitasaidia kutoa jamii iliyo bora .

Wakichangia mada katika mkutano huo washiriki wamesema tatizo  kubwa linalowkabili ni jamii kutokuwa na imani juu ya utekelezaji wa dhana ya utawala bora.

Comments are closed.