WAKULIMA WAMESHAURIWA KUFUATA MAELEKEZO YA KITAALAMU WANAYOPEWA NA MABWANA SHAMBA

Wakulima wameshauriwa kufuata maelekezo ya kitaalamu wanayopewa na mabwana shamba ili kuzalisha mazao bora.

Akizungumza na wakulima katika kongamano la wanachama  wa taha mkurugenzi mtendaji  wa taha ndg Jacline Mkindi amesema wakizalisha mazao yenye kiwango wataweza kutangaza biashara zao katika masoko ya nje.

Mwakilishi wa TAHA Zanzibar Omar Abdallah Moh’d amesema kuwa ni vyema wakulima hao kuweka kumbukumbu ya mauzo ya bidhaa wanazofanya ili kujua faida na hasara wanayoipata.

baadhi ya wakulima hao wamesema tangu walipojiunga na taha wamefaidika kwa kuzalisha mazao yenye ubora na yanayohitajika katika soko.

 

 

 

 

 

Comments are closed.

error: Content is protected !!