WAKULIMA WAMEIOMBA WIZARA YA KILIMO KUWASAIDIA KUPATA DAWA ZA KUONDOSHA MARADHI KWA KILIMO CHAO

Wakulima wanaolima mboga mboga katika eneo la migombani jeshini  wameiomba wizara ya kilimo kuwasaidia kupata dawa  itakayosaidia kuondosha maradhi  yanayoharibu kilimo chao.

Wakizungumza na zbc  wakulima hao wamesema wamekuwa wakitumia nguvu nyingi katika kilimo hicho lakini mafanikio wanayoyapata ni madogo kutokana na mboga zao  kunyauka kabla ya kufika wakati wa kuvuna.

Wamesema tatizo hilo ni la muda mrefu  na ufumbuzi wake hawajaupata  licha ya jitihada wanazozichukuwa  za kutafuta wataalam.

Wakati huo huo akina mama wanaojishughulisha na ufugaji wa kuku katika shehia ya mtende wilaya kusini unguja  wamesema  wizi wa kuibiwa mifugo yao unawafanya kutofikia malengo waliyojipangia.

Naibu sheha wa shehia ya mtende  amethibitisha kuwepo kwa wizi huo na kusema  katika kupambanda na tabia hiyo imeanzishwa kamati ya ulinzi na usalama ili kuhakikisha inakomesha vitendo hivyo sambamaba na  uovu mwengine wowote.

 

Comments are closed.

error: Content is protected !!