WAKULIMA WA ZAO LA KARAFUU WAMEWATAKA KUUZA MAKONYO YAO KATIKA SHIRIKA LA BIASHARA LA TAIFA LA ZSTC

Waziri wa Biashara  na Viwanda  Balozi Amina Salim Ali amewataka Wananchi na Wakulima wa zao la Karafuu kuuza makonyo yao katika Shirika la Biashara la Taifa  ZSTC  kwa maslahi yao na Taifa kwa ujumla.

Balozi Amina ameyasema hayo katika ukumbi wa Kiwanda cha Makonyo Wawi wakati alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya  mavuno ya Karafuu yanayoendelea katika msimu  huu wa Mvua za Vuli .

Pia Balozi Amina amewasisitiza Wananchi kutojihusisha na suala la ununuzi wa Karafuu kwa njia ya  Vikombe, kwani atakaebainika hatua za   Sheria itachukuliwa dhidi yake.

 

Comments are closed.

error: Content is protected !!