WAKALA WA MKONGA ZANZIBAR WATAKIWA KUFANYA KAZI ZAO KWA MUJIBU WA TARATIBU ZA SERIKALI

Waziri wa ujenzi mawasiliano na usafirishaji Mhe Dkt Sira Ubwa Mamboya ameitaka bodi ya ushauri wa wakala wa mkonga zanzibar kufanya kazi zao kwa mujibu wa taratibu za serikali zilizopo.

Mhe Waziri ameyasema hayo alipokuwa akizundua rasmi bodi hiyo huko katika ukumbi wa mikutano wa wizara ya ujenzi kisauni nje kidogo wa mji Zanzibar.

Dkt Sira amesema matumaini yake ni kuwa bodi hiyo itaendelea kumshauri na kupendekeza mambo yanayofaaa kwa manufaa ya umma na kuitaka bodi hiyo kutunza siri pamoja na kufanya kazi kwa uaminifu na uweledi ili kufanikisha malengo yaliyopo.

Mwenyekiti wa bodi hiyo Dkt Haji Ali Haji ameahidi kuwa watafanya kazi kwa uwaminifu na uweledi mkubwa ili kufikia malengo ya uchumi wa kati, mkuza namba lll pamoja na kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi kama inavyoagizwa na rais wa zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi.

Nae mkurugenzi utumishi na uwendeshaji wa wizara ya ujenzi mawasiliano na usafirishaji ndugu Bimkubwa Abdi Nassib alitoa nasaha zake kwa bodi hiyo kwa kuishauri kufuata miongozo ya kazi zao na kutomuangusha mhe rais  kwa imani waliyopewa.

Comments are closed.

error: Content is protected !!