WAKALA WA CHAKULA NA DAWA ZANZIBAR IMETEKETEZA JUMLA YA TANI 25 ZA MCHELE NA TANI TATU ZA DAWA

Wakala wa Chakula na Dawa Zanzibar imeteketeza  umla ya tani 25 za Mchele na tani tatu za Dawa na bidhaa nyengine zisizofaa kwa Matumizi ya Binaadamu.

Akizungumza katika kazi ya kuteketeza bidhaa hizo Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti wa Usalama wa chakula dkt Khamis Ali Omar amesema bidhaa hizo zimeharibika kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo kuingia maji ya Chumvi na bidhaa hizo kutokuwa salama kwa Afya ya watumiaji.

Amesema wakala huo utahakikisha Wananchi wanatumia bidhaa zenye kiwango hivyo wamewataka Wananchi kutoa ushirikiano kwa kutoa Taarifa wanapoziona bidhaa zenye mashaka.

Afisa usimamizi wa Usalama na ubora wa Dawa wa wakala huo nd. Nasir Buheti amewataka Wafanyabiashara kufuata utaratibu katika uingizaji wa bidhaa Nchini ili kuwalinda watumiaji na wao kuepuka hasara.

 

Comments are closed.