WAHITIMU WA SHAHADA YA KWANZA CHUO CHA UTAWALA WA UMMA WAMETAKIWA KUTUMIA VYEMA TAALUMA WALIOIPATA

Chuo cha Utawala wa Ummma (IPA ) kimewataka Wanafunzi wa Chuo hicho kuzingatia Taaluma wanayoipata ili kuitumia kwa Ufanisi katika  Ufanyaji Kazi.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi  Idara ya Miundo  ya Tasisi  Utumishi  na Utawala Bora Nd.Shaibu Ali  wakati  Akizungumza na  Wahitimu  waliomaliza Masomo ya  Utunzaji wa Kumbukumbu na Nyaraka katika Chuo hicho Ngazi ya Shahada ya Kwanza.

Amesema Taaluma ya kuweka vyema Kumbukumbu ina umuhimu mkubwa kwani inatunza Nyaraka mbalimbali za Serikali.

Mrajisi wa  Chuo hicho  Nd.Mshauri Abdalla Khamis amesema  Wahitimu hao wanapaswa kulete mabadiliko  katika Taasisi zao kupitia Masomo waliyosoma .

Akisoma Risala  Muhitimu Nd.Hadia  Ramadhani Amesema Chuo hicho kinaukosefu wa Vifaa vya kufanyia Kazi na Kuiomba Serikali kujitahidi kuwapatia Vifaa hivyo ili Wanafunzi  waweze Kusoma kwa Uweledi zaidi.

 

Comments are closed.

error: Content is protected !!