WAGOMBEA WA VYAMA VYA SIASA WATOA SHUKURANI BAADA YA MATOKEO YA URAIS

Rais Mteule wa Zanzibar Dk. Hussein Mwinyi amewahimiza Wazanzibari kuendelea kuwa kitu kimoja katika kujenga Zanzibar mpya.

Akizungumza baada ya kutangazwa Mshindi wa Urais wa Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu huko Maruhubi, Dk. mwinyi ameahidi kuendeleza mema na kujenga Imani kwa Wananchi.

Amesema baada ya Uchaguzi kumalizika Jukumu kubwa lililobakia ni kuhakikisha Wananchi wanakuwa kitu kimoja kufanya kazi za Maendeleo.

Dk. Mwinyi aliyechaguliwa kuongoza Awamu ya Nane ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar amesema anakishukuru chama cha Mapinduzi na Wanachama wake kwa kuamini kumpa ridhaa na kuahidi kutowaangusha.

Wakati huo huoakizungumza kwa niaba ya Wagombea wenzake Mgombea wa Ada Tadea nd. Juma Ali Khatibu amewashukuru Wananchi wa Zanzibar kwa kufanya Uchaguzi wa Kistarabu na wao kwa ujumla wamekubaliana na Matokeo ya Uchaguzi na kuwataka Wapinzani wote kumuunga Mkono Rais Mteule Dk. Hussein Mwinyi kufanya kazi za kuleta Maendeleo.

Comments are closed.