WAFANYA BIASHARA WA SOKO LA KWEREKWE WAMETAKIWA KUTOWA USHIRIKIANO KATIKA KUDUMISHA USAFI

Mkuu wa Soko la mwanakwerekwe Nd. Mcha Ussi Mcha amewataka wafanyabiashara wa Soko hilo kutowa ushirikiano katika kudumisha usafi ili kulifanya Soko  liwe safi na lenye mandhari nzuri.

Akizungumza na ZBC ofisini kwake Mwanakwerekwe Nd. Mcha amesema suala la kudumisha usafi si la Manispaa pekee hivyo kila mfanya biashara anapaswa kuyatunza mazingira katika eneo lake la kazi na kuepuka kuyachafua kwa makusudi kwa kisingizio cha tozo hafifu wanalotoa.

Akielezea suala la miundo mbinu za Soko  hilo ikiwemo mitaro ya kupitishia maji amesema hali ilioko sasa hairidhishi na kuwataka Wananchi kuwa wastahamilivu kwani Serikali iko katika mikakati ya kuliboresha Soko hilo  liwe la kisasa.

Kwa upande wake mfanya biashara wa Soko hilo Nd. Suleiman Salum Suleiman amesema kupanda kwa bidhaa mbali mbali inatokana na upungufu wa bidhaa hizo na pindi zinapokuwa nyingi bei hizo hupunguwa hivyo amewata Wananchi kukubaliana na hali iliopo kwa muda hadi biadhaa hizo zitakapopatikana kwa wingi.

Nae mama lishe anaepika chakula katika Soko hilo Nd. Aisha Ramadhan amesema kupanda kwa tungule, mbatata, vitunguu maji na karoti kunapelekea ugumu katika manunuzi ya viungo hivyo kwa ajili ya shughuli za mapishi na kupelekea kukosa faida kwani huwabidi kuuza chakula chao kwa bei  ya kawaida.

 

Comments are closed.

error: Content is protected !!