VIONGOZI WA DINI KUSIMAMIA IMARA KWA LENGO LA KUEPUSHA MIFARAKANO YA KISIASA KATIKA NYUMBA ZA IBADA

Katibu  Mkuu  wa  Chama  cha  Mapinduzi    Dr. Bashiru  ali  kakurwa    amewaasa   viongozi  wa  dini   kusimama  imara  kwa  lengo  la  kuepusha   mifarakano   ya  kisiasa   katika  nyumba  za  ibada.

Tamko  hilo  amelitoa  wakati   akizungumza   na   Baraza  la  Wazee  wa CCM Zanzibar   katika   Afisi  Kuu  ya   CCM   Kisiwandui   juu  ya  muelekeo  wa  kampeni  na  msimamo  wa  Chama  hicho   kufuatia  matukio  ya  uvunjifu  wa   amani   na  mashambulizi  yanayo fanywa  dhidi  ya  Wanachama  wa  chama  hicho  katika  maeneo  tofauti  ya  Nchi.

Dr   Bashiru   amesema   CCM  imestushwa   na  kulaani  vikali   matukio   hayo   lakini  kamwe  haijipangi  kulipa  kisasi  kwani  chama  hicho  kinaongozwa  kwa  kuzingatia   katiba,   uongozi  bora   pamoja  na  kuheshimu  Sheria  za   Nchi .

Katibu  Mkuu  Bashiru  amewahakikishia   Wazee  wa  Chama  cha  Mapinduzi  kuwa   chama  hicho  kitashinda  uchaguzi  mkuu  ujao  kutokana   na   kusema  ukweli  kwa  Wananchi   , kuwa  na  sera  bora

Na  zinazotekelezeka    na   kusimamisha   wagombea   wenye  sifa  za Uongozi.

 

Katika  Mkutano  huo  katibu  Mkuu  wa CCM   amekabidhi  ilani  ya  Uchaguzi   kwa   wazee  wa  ccm    na  kuwasisitiza   kuendelea   kuwa  bega  kwa  bega  na  Wagombea  wa  chama  hicho  hadi   ushindi.

Comments are closed.

error: Content is protected !!