VILABU SITA VINAVYOTARAJIWA KUSHIRIKI KOMBE LA MAPINDUZI VIMEPATIWA VIFAA KWA AJILI YA MICHUANO

Vilabu Sita vya Soka vya Zanzibar zinazotarajiwa kushiriki Kombe la Mapinduzi zimepatiwa vifaa kwa ajili ya Michuano hiyo inayotarajiwa kuanza Januari 2021.

Akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kukabidhi vifaa hiyo Mkuu wa kitengo cha Masoko Nevili mchata amesema lengo la kampuni hiyo kuja Zanzibar ni kutanganza bidhaa zao za michezo na kuchangia juhudi za SMZ za kuinua sekta hiyo.

Viongozi wa Vilabu hivyo wamesema msaada huo utawasaidia kushiriki kwa mafanikio katika michuano ya kombe la Mapinduzi,na kuziomba Kampuni nyengine kujitokeza kusaidia timu hizo ili kuyaenzi mapinduzi ya mwaka 1964.

Vilabu vilivyo kabidhiwa vifaa hivyo ni Malindi,mlandege za Unguja na ,Jamuhuri na Chipukizi za Pemba.

 

Comments are closed.

error: Content is protected !!