VIJANA WALIOPATIWA MIKOPO YA ELIMU YA JUU WATAKIWA KUREJESHA FEDHA HIZO KWA WAKATI

Afisa mdhamini Wizara ya elimu na mafunzo ya amali Mohamed Nassor amewataka vijana waliopata mikopo ya elimu ya juu kurejesha fedha hizo ili ziwanufaishe wanafunzi wengine.

Akifungua mafunzo mkutano wa kujadili mikakati ya urejeshaji wa mikopo kwa maafisa utumishi na wahasibu katika ukumbi wa Baraza la mji Chake Chake, mdhamini Mohamed amesema marejesho ya mikopo hiyo  hayaridhishi.

Kwa upande wake mratibu wa bodi ya mikopo ya elimu ya juu Zanzibar ofisi ya Pemba Ahmada Omar Juma amesema mashirikiano yanahitajika kwa kila taasisi ili wanaodaiwa warejeshe fedha hizo kwa wakati.

Akiwasilisha mada ya marejesho ya mikopo, meneja wa mikopo Abudu Issa Khamis amesema wadaiwa 2,648 wanafuatiliwa ili waanze marejesho ya mikopo yao.

Nao washiriki wa mkutano huo wameishauri bodi ya mikopo kufanya ufuatiliaji wa mara kwa mara maofisini na wasisubiri kupelekewa taarifa ofisini kwao.

 

 

Comments are closed.

error: Content is protected !!