VIJANA WA JESHI LA KUJENGA TAIFA JKT WALIOJITOLEA KURIPOTI KATIKA KAMBI YA JKT MGULANI

Jeshi la wananchi wa Tanzania JWTZ limewataka vijana wa jeshi la kujenga taifa JKT waliojitolea katika operesheni ya ujenzi wa ukuta unaozunguka eneo la mgodi wa madini ya Tanzanite mererani kuripoti katika kambi ya jkt mgulani ili kukamilisha taratibu za ajira.

Mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama Jenerali Venance Mabeho amezungumza na waandishi wa habari ngome jijini Dar-es-salaam na kusema hatua hiyo ya kuwaajiri vijana hao ni utekelezaji wa ahadi ya amiri jeshi mkuu na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli aliyoitoa tarehe 12 mwezi septemba 2017 wakati akizindua ukuta  huo wa wamererani arusha.

Jenerali Mabeho amesema chini ya usimamizi wa timu ya waandisi ujenzi kutoka JWTZ vijana hao waliweza kukamilisha kazi ya ujenzi wa ukuta katika eneo la mgodi ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Magufuli alilolitoa tarehe 6 april 2018 wakati akizindua barabara ya kia lakini baadhi yao bado hawakuajiliwa.

Jenerali Mabeho ameukumbusha watanzania kuwa madhumuni ya kuwaandikisha vijana JKT  ni kuwafundisha uzalendo na kuwajengea uwezo wa stadi za kazi ili waweze kujitegemea tofauti na dhana iliyojengeka sasa kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwapatia ajira.                               .                                                         .

Aidha Jenerali Mabeho amesema Rais Magufuli amefanya mabadiliko kidogo ya uongozi ambapo amemteua brigedia Jenerali Charles mbunge kuwa mkuuu wa JKT na kumteua meja Jenerali Martine Busungu kuwa mkuu wa tawi la jeshi la akiba

Comments are closed.

error: Content is protected !!