VIJANA KUWA WABUNIFU WA KUTAFUTA NJIA ZA KUTATUA CHANGAMOTOYA UKOSEFU WA AJIRA

Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mhe Lela Mussa amehimiza vijana kuwa wabunifu wa kutafuta njia za kutatua changamoto mbali mbali zinazowakali ikiwemo ya ukosefu wa Ajira.

Ameeleza hayo katika ukumbu wa Chuo Kikuu cha Taifa zanzibar SUZA  Maruhubi wakati akifungua masindano ya ubunifu wa kuibua vipaji vya kutatua changamo katika Jamii .

Amesema Pamoja na kuwa wabunifu wa kutatua changamoto hizo Waziri pia amewataka vijana Nchini kuacha Uzembe wa kila aina ikiwa ni pamoja na kuepuka kutumia dawa za kulevya hali inayowasababishia kutokuwa na malengo ya maendeleo. Makamu mkuu wa chuo cha SUZA bi Zakia Abuubakar amesema mashindano kama hayo yanapaswa kuvishirikisha vyuo mbali mbali Nchini.

Mratibu wa mashindano hayo Bw, Saidi Yunus amesema mashindano ya namna hiyo ni muhimu kwa Wanafunzi na vijana kwani yanawawezesha kuwa Wataalamu wa kutafuta njia za kuondoa shida zao.

Comments are closed.