UTAYARI WA SERIKALI YA AWAMU YA NANE KATIKA KUSHIRIKIANA NA BENKI YA NMB KWA KUIMARISHA UCHUMI

is wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Dk hussein Ali Mwinyi ameeleza  Utayari wa serikali ya Awamu ya nane katika kushirikiana na  Benki ya NMB kwa ajili ya kuimarisha uchumi pamoja na huduma za kijamii Zanzibar.

Hayo ameyasema leo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa Benki ya nmb ikulu jijini zanzibar ukiongozwa na Afisa mtendaji Mkuu wa benki hiyo Bi Ruth Zaipuna .

Katika maelezo yake Rais dk. hussein alisema kuwa Benki ya nmb imepata mafanikio makubwa hivyo, Serikali anayoiongoza iko tayari kushirikiana na Benki hiyo katika kuimarisha miradi mbali mbali ya kiuchumi sambamba na huduma za kijamii.

Alisema kuwa katika kuendeleza na kuimarisha Miradi ya maendeleo ikiwemo afya na Elimu Serikali anayoiongoza iko tayari kutoa ushirikiano wake kwa benki hiyo ili iweze kuunga mkono juhudi za serikali katika sekta hizo ambazo wamekuwa wakitoa misaada yao.

Rais Dk. Hussein alisema kuwa Serikali iko tayari kukopa fedha kwa ajili ya kuwatafutia maeneo  Wajasiriamali ili iweze kuwasaidia katika kufanya shughuli zao.

Comments are closed.