USTAWI WA SEKTA YA KILIMO UTASAIDIA KUINASUA TANZANIA

Naibu waziri wa viwanda biashara na uwekezaji mhandisi stela manyanya amebainisha hilo katika mkutano wa wadau wa kilimo na viwanda uliyofanyika jijini dar es salaam ambapo amesema ustawi wa sekta ya kilimo utasaidia kuinasua tanzania kutokana na changamoto ya kuagiza bidhaa kutoka  nje .

Amebainisha kuwa dhamira ya serikali ya kufufua viwanda vilivyokufa na kuanzisha viwnada vipya inalenga kutumia malighafi za kilimo za zinazozalishwa hapa nchini.

Mkurugenzi wa jukwaa la wadau wa sekta ya kilimo (ansaf) audax rukonge amesema ili kufikia adhma ya uwekezaji katika sekta ya viwanda ni vyema kuwa na namna bora ya kuwasaidia wazalishaji wadogo katika sekta ya miundominu ya maji, nishati na barabara ili uwekwzaji uweze kuleta tija.

Mada mbalimbali ziliwasilishwa katika mkutano huo wa siku2 ulioandaliwa na jukwaa la wa sekta ya kilimo ansaf umewakutanisha wadau wa sekta za kilimo na viwanda.

No Comments Yet.

Leave a comment