UJASIRIAMALI NDIO NJIA MBADALA YA KUONDOSHA TATIZO LA AJIRA LINALOWAKABILIA WANANCHI HASA VIJANA

Afisa mdhamini wizara ya kazi uwezeshaji wazee wanawake na watoto Khatibu Vuai Shein amesema sekta ya ujasiriamali ndio njia mbadala ya kuondosha tatizo la ajira linalowakabilia wananchi hasa vijana

Mdhamini Hakimu Vuai Shein amesema hayo Wizarani kwake Gombani wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo maafisa watakaotowa huduma kwa wajasiriamali katika vituo vya wilaya, yanayowashirikisha maafisa ushirika, vijana, ustawi wa wilaya pamoja na wajasiriamali.

Amesema serikali imeweka fursa na mipango bora ya kuwawezesha wananchi kujiajiri katika sekta ya ujasiriamali kwenye nyanja tofauti kwa kutoa mikopo yenye masharti nafuu ili kuondosha tatizo la mitaji.

Aidha Mdhamini shein ameitumia fursa hiyo, kuwataka washiriki hao kuzitumia nafasi walizonazo kupiga vita vitendo ya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia kwa wanawake na watoto ambalo linaathiri jamii na taifa.

Akielezea lengo la mafunzo hayo Kaimu Mratibu Idara ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Amini Omar Ali amesema ni kujenga uwezo kwa washiriki hao ili watowe huduma bora kwa jamii, kwani ina mahitaji makubwa ya ajira.

Jumla ya mada tatu zimewasilishwa katika mafunzo hayo na washiriki kubainisha fursa zinazopatika katika uzalishaji

Comments are closed.

error: Content is protected !!