UCHUMI WA ZANZIBAR ULITETEREKA KUFUATIA KUZUILIWA KUINGIA KWA WATALII KUTOKANA NA CORONA

Waziri wa  Habari  Utalii  na  Mambo  ya Kale  Mh. Mahmoud Thabit  Kombo  amesema  Uchumi wa  Zanzibar  ulitetereka kwa asilimia 30  kufuatia  kuzuiliwa  kuingia kwa  Watalii  kutokana na  Maambukizi ya  CORONA na kudumaza  Sekta  ya  Utalii.

Akizungumza  katika  kipindi  cha  moja  kwa  moja  cha  Alasiri  yetu  hapa  ZBC  amefahamisha  kuwa  katika  muda  huo  mapato  yanayotokana  na  Fedha  za  Nje  yalipungua  kwa  asilimia  80  na  kuathiri  Nyanja  zote  za  Kiuchumi  .

Amesema Uamuzi wa  Serikali ya  Mapinduzi  ya Zanzibar  wa  kufungua  Milango ya  Utalii  ikiwemo  Anga  na  Bandari  na  kuwa  tayari  kupokea  wageni  kunalenga  kuurejesha  Utalii  katika  kiwango  chake  na  kwamba  Serikali  imechukua  Hatua  zote  muhimu  za  kudhibiti  Maambukizi  mapya  ya CORONA katika  maeneo  yote  .

Mhe.  Mahmoud  amesema  katika  muda  huo  imegundulika  kuwa  upo  umuhimu  Mkubwa  wa  kuutangaza  Utalii  wa  ndani   kwani  kutegemea  wageni  pekee  kutoka  mataifa  ya Ulaya  kunaweza  kukaathiri  Sekta  hiyo  pale Dunia  inapopatwa  na  Majanga  .

Amesisitiza  kuwa  Serikali  imedhamiria  kurejesha  kiwango  cha  Idadi ya  Watalii  wanaoingia  Nchini  angalau  kwa  asilimia  30 kila  mwezi  ili   kufikia  Watalii  548 ,000 waloingia  Nchini  mwaka  uliopita  kabla ya  kuripuka  kwa  Maambukizi  ya  CORONA.

Comments are closed.

error: Content is protected !!