UADILIFU NA UMAKINI WA VIONGOZI WANAOSIMAMIA JUMUIYA ZA CHAMA ITAENDELEZA KUIMARISHA KATIBA NA ILANI

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM  Balozi Seif Ali Iddi amesema Uadilifu na Umakini wa Viongozi wanaosimamia Jumuiya za Chama itaendeleza kuimarisha Chama hicho katika utekelezaji wa Katiba na Ilani yake.

Amesema CCM imekuwa kinapata Heshima kubwa na kuungwa mkono na Wananchi wengi  kutokana na kutekeleza kwa  Vitendo ilani na Sera zake na kuwafanya Wanachama na Viongozi wa Vyama vya Upinzani kuridhika kujiunga na Chama hicho Kikongwe Barani Afrika.

Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo katika Ofisi yake iliyomo ndani ya jengo la Baraza la Wawakilishi Chukwani wakati wa mazungumzo yake na Ujumbe wa Viongozi Wakuu wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania ilioongozwa na Mwenyekiti wake Mheshimiwa Edmund Bernad Mndolwa.

Alisema Changamoto zilizokuwa zikijichomoza ndani ya Jumuiya za chama cha Mapinduzi ambazo ziliwahushisha baadhi ya Wanachama na hata Viongozi wake kwa sasa hazistahiki kupewa Nafasi hasa ikizingatiwa kwamba Chama cha Mapinduzi katika miaka ya sasa kinaendeleshwa katika Mfumo wa Kisayansi.

Balozi Seif ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliueleza Ujumbe wa Viongozi hao wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania kwamba Taasisi hiyo imebarikiwa kuwa na Rasilmali nyingi ikilinganishwa na Jumuiya nyengine za Chama Bahati ambayo lazima waizingatie na kuisimamia ipasavyo ili lile lengo la kuanzishwa kwake lifikie pazuri.

Mapema Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Mheshimiwa Edmund Bernad Mndolwa alisema Uongoziwa Taasisi hiyo ya Chama hivi sasa uko katika Mchakato wa kuhakikisha CCM inaendelea kushika hatamu katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika baadae mwaka huu.

Mheshimiwa Edmund alisema Viongozi wa Jumuiya hiyo wanaendelea na mikakati ya muda mfupi na mrefu katika kuona malengo hayo yanatimia na kuleta mafanikio waliyoyalenga.

Naye kwa upande wa Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Visiwani Zanzibar nd. Haidar Haji Abdullah alisema suala la usafiri linapaswa kuangaliwa na kupewa msukumo mkubwa ili kuondoa changamoto inayowakabili Viongozi wa Jumuiya hiyo kwa upande wa Zanzibar.

 

Comments are closed.