TAASISI YA MICHEZO YA ZEST KWA KUSHIRIKIANA NA CHAMA CHA MPIRA WA KIKAPU

Taasisi ya michezo ya zest kwa kushirikiana na chama cha mpira wa kikapu cha nchini denmark  wameitimisha mafunzo ya siku nne ya ukocha na pamoja na waamuzi ya mchezo huo.

mafunzo hayo yaliyofanyika katika viwanja vya skuli vikokotoni yameambatana na utoaji vyeti ngazi cartificate kwa makocha na waamuzi.

Mwanasheria wa wizala ya vijana  utamaduni sanaa na michezo Saidi Maliki amezungumza na zbc michezo ameseam taasisi ya zest kwa kushirikiana na chama cha mpira wa kikapu zanzibar wamefanya jambo ambalo kwa sasa taifa linahitaji kupata wlimu bora wa mchezo pamoja na waamuzi wenye taaluma.

Kocha wa new west Bw.Nassoro Salumu, amesema ipo haja ya makocha waliopata taaluma hiyo kuweza kusaidia vijana na kuunyanyuwa mchezo huo.

Mkurugenzi wa taasisi ya michezo zest,pamoja na wakufunzi wa mpira wa kikapu kutoka denmark wamesema wamesema kutowa mafunzo hayo ni sehemu ya kutimiza malengo ya vijana.

No Comments Yet.

Leave a comment