SUKARI DAR BADO NI TATIZO

Upatikanaji wa Bidhaa ya Sukari katika Jiji la Dar es salaam bado ni tatizo kutokana na baadhi ya Wafanyabiashara kuuza kwa Shilingi Elfu tatu hadi Elfu nne badala ya Shilingi Elfu mbili mia sita kwa kilo.

Wakizungumza na ZBC  baadhi ya Wakazi wa Jiji la Dar es salaam wamesema hali hiyo imepelekea kushindwa kununua bidhaa hiyo muhimu hususani katika kipindi hicho cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Nao baadhi ya Wafanyabiashara Wamesema baada ya kutangazwa kwa Bei elekezi  ya upatikanaji wa bidhaa hiyo umekuwa ni washida katika  Maduka  ya Jumla.

ZBC ilipita katika Maduka ya Jumla ya kuuza Sukari Jijini hapo nakushuhudia Matangazo katika Maduka hayo yakionyesha kutopatikana na Bidhaa hiyo.

Ikumbukwe hivi karibuni Serikali ilitangaza Bei elekezi ya Uuzaji wa Sukari Nchini ambapo kwa Mkoa Dar es salaam inatakiwa kuuzwa kwa Shilingi Elfu Mbili na Mia Sita na Shilingi Elfu tatu na mia mbili kwa baadhi ya Maeneo ya Nchi.

Comments are closed.

error: Content is protected !!