SMZ KUWEKEZA KATIKA KUWAINUA WAFANYA BIASHARA WADOGO WADOGO NCHINI

Waziri wa Biashara na Viwanda Mh.Amina Salum Ali amesema Serikali imeamua kuwekeza katika kuwainua Wajasiria mali wadogo wadogo hususan waanikaji wa Dagaa.
Akizungumza na Wajasiriamali wa uanikaji wa Dagaa wa Fungu refu Mkoa wa Kaskazini Unguja amesema Serikali imeamua kufanya hivyo kwa kutambua umuhimu wa Biashara ya Dagaa inavyokuwa Siku hadi Siku na kuona jitihada zianazochukuliwa na Wajasiriamali hao katika kujikwamua Kiuchumi.
Mh.Amina amesema kupitia Wakala wa maendeleo ya Viwanda vidogo vidogo na vya kati Smida kuwasaidia Wajasiriamali hao kwa kuwajengea Diko ambalo litaendana na shughuli zao za Kiuchumi.
Mkurugenzi wa Wakala wa Maendeleo ya Viwanda vidogo vidogo na vya kati Nd.Haji Abdulhamid amesema lengo la Smida ni kuwainua Wajasiriamali Kiuchumi na kuwapatia mitaji itakayowasaidia kuimarisha mazingira yao ya Biashara.
Wajasiriamali hao wameishukuru Serikali kwa jitahada ambazo inazichukuwa katika kuwaunga Mkono katika harakati zao za Maendeleo .

Comments are closed.