SERIKALI YANUNUA MASHINE YA UCHUNGUZI YA VINASABA.

Askari Polisi, Madaktari na watendaji wa Afisi ya Mkemia Mkuu wa maabara ya Merikali wametakiwa kushirikiana ili kutoa matokeo sahihi ya uchunguzi wa sampuli za matukio mbali mbali yanayoripotiwa.

Mkemia Mkuu wa Serikali Silim Rashid  amesema ushirkiano na umakini katika kazi hiyo kutaepusha kutolewa majibu ya uchunguzi yasiyo sahihi.

Akifunga mafunzo kwa maafisa wa uchukuaji wa sampuli kwa wtendaji hao hasa ukizingatia amesema Serikali imenunua mashine ya uchunguzi ya vinasaba dna kwa gharama kubwa hivyo ni muhimu kuwepo uadilifu katika kazi.

Washiriki wa mafunzo hayo yaliyohusisha kanuni ya huduma za vinasaba na uchukuaji wa vinasaba wameomba kupatiwa vitendea kazi vya kutosha ili wafanikishe majukumu yao kwa umakini.

 

Comments are closed.

error: Content is protected !!