SERIKALI YA UINGEREZA KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

Makamu wa kwanza wa Rais Mhe. Othman Masoud Othman amesema Serikali imekubaliana kufanya kazi kwa pamoja na Serikali ya uingereza katika mapambano dhidi ya uhalifu wa kidunia ikiwemo dawa za kulevya kwa lengo la kuinusuru jamii ya Zanzibar

Ameyasema hayo wakati alipofanya mazungumzo na Balozi msaidizi wa uingereza Nchini Tanzania Rick shearn wakati alipofika kwa ajili ya kujitambulisha na kuonesha adhma ya Serikali ya Uingereza kuendelea kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Amesema kuna mambo yanaendelea kuiathiri Dunia hasa suala la Dawa za kulevya, ufichwaji wa  Fedha za kihalifu ambapo Serikali imekubaliana kupitia Vyombo mbali mbali vikiwemo vinavyohusika na usimamizi wa sheria, uchunguzi, na usimamizi wa kodi.

Wakati huo huo Mhe. Othman amekutana na Mwakilishi mkaazi wa UNICEF Tanzania Shalin Bahuguna ambapo wameihakikishia Serikali ushirikiano kuona Zanzibar inaendelea kuwa vyema katika masuala ya Afya.

Mhe. Othman amemuhakikishia muakilishi huyo kuwa Serikali itaendelea kuungana nao pamoja katika kuhakikisha Jamii ya Zanzibar inakuwa na ustwi mzuri hasa katika suala la Afya.

 

 

Comments are closed.