SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR IMETANGAZA KUWEPO KWA MGONJWA MWENGINE WA MARADHI YA CORONA

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetangaza kuwepo kwa Mgonjwa mwengine wa Maradhi yaCORONA na kufanya idadi ya Wagonjwa hao hapa Zanzibar kuwa wawili .

Akitoa taarifa hiyo Waziri wa Afya Mh. Hamad Rashid Muhammed amesema Mgonjwa huyo ambae ni Raia wa Ujerumani alikuwa katika Kambi maalum ya washukiwa wa Virusi vya CORONA huko Kidimni  baada ya Mume wake kugunduliwa kuwa na Virusi hivyo.

Katika hatua nyengine Wizara ya Afya Zanzibar imeifunga Duka la Dawa la  Aban Care liopo Fumba kutokana na kukamatwa kwa  baadhi ya vifaa vya tiba vinavyouzwa kinyume na Sheria.

Aidha Wizara ya Afya Zanzibar imewakumbusha Wananchi wa Zanzibar kuendelea kuchukua tahadhari juu ya janga hatari la maradhi ya CORONA liloikumba Dunia .

 

Comments are closed.

error: Content is protected !!