SERIKALI IMESHAURIWA KUCHUKUWA HATUA WATAKAOBAINIKA KUFANYA UBADHIRIFU WA FEDHA ZA UMMA

Chama cha Mapinduzi kimeishauri Serikali kuchukuwa hatua  dhidi ya Watendaji wa Umma watakaobainika kufanya  ubadhirifu wa Fedha za umma kufuatia Ripoti ya Mkaguzi  Mkuu wa Hesabu za serikali iliotolewa hivi karibuni.

Tamko  hilo  limetolewa  na   Katibu  wa   Idara  ya Siasa   Itikadi  na  Uenezi  ya CCM  Zanzibar  bi. Catherine  Peter  Nao   wakati  akizungumza  na   Vyombo  vya  Habari   siku tatu baada  ya   kuwasilishwa  kwa    Ripoti  hiyo  Serikalini  .

Amefahamisha   kuwa  CCM Zanzibar   imestushwa   na  ubadhirifu   wa  kiwango  kikubwa  cha  Fedha  za  umma  ambazo  zingewezesha  kufanyika  kwa  mipango   mingi  ya  maendeleo  ikiwemo  kuimarika  kwa  mindo mbinu  ya  Maji  ,  Afya ,   Elimu  na   Kilimo  lakini  zimeishia  kwa    watendaji  wachache   wasio   na  uadilifu  na   kuipongeza Serikali  kwa   kuiweka  wazi  Ripoti   hiyo.

Wakati  huo  huo   CCM   imeeeleza  kutoridhika    na   kasi    ya   baadhi  ya    Mawaziri   kwa  kutoendana na maagizo   na  malengo  ya    Serikali    yaliyotolewa   na    Rais  wa  Zanzibar  na   Mwenyekiti  wa   Baraza  la  Mapinduzi   Dr.Hussein   Ali  Mwinyi   wakati   akiwaapisha   Mawaziri   ikiwemo   kuwafikia   wadau   na   kushuka  kwa   Wananchi  kusikiliza  matatizo   yanayowakabili.

Katibu  Cathirine   amesisitiza  kuwa   Chama  Cha  Mapinduzi  kitaendelea   kuunga  mkono  juhudi  za   Serikali   za   kusimamia  uwajibikaji,  matumizi   sahihi  ya  Fedha  za  umma   na  mapambano dhidi  ya   ufisadi.

 

Comments are closed.